Wawekezaji kutoka Uganda waonyesha nia ya kuwekeza katika miradi ya umeme Tanzania

Na Zuena Msuya, Dodoma Waziri wa Nishati Mhe. January Makamba amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uganda nchini Tanzania pamoja na wawekezaji kutoka nchini humo kuhusu kuwekeza katika mradi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Lindi, Masasi, Tunduru na Songea. Mazungumzo hayo yamefanyika Machi 21, 2023 katika ofisi za Wizara ya Nishati mkoani Dodoma